SIKU 4: SABASABA YA DHAHABU.
Ni siku njema tena katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba)
Leo, Julai 1, 2026, Banda la Wizara ya Nishati limeanza siku kwa kumpokea mgeni wake wa kwanza, Bi. Ester Mashaka Msengi, mkazi wa Kibaha Mjini, mkoani Pwani.
Akiwa na tabasamu na shauku ya kujifunza, Bi. Ester alipata maelezo kuhusu Nishati Safi ya Kupikia kutoka kwa Mtaalam wa Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia, Bi. Amina Almasi, chini ya uangalizi wa karibu wa Mhandisi wa Nishati, Zahoro Rashid.
Baada ya kupata elimu hiyo, Bi. Ester aliondoka akiwa na furaha na kuridhishwa na maarifa aliyoyapata kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na fursa mbalimbali zinazotolewa na Sekta ya Nishati.
Na wewe unakaribishwa kutembelea Banda la Wizara ya Nishati lililopo karibu na jengo la TANESCO katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, na ujifunze kuhusu huduma, miradi na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya nishati.