Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

TAASISI YA UTAFITI YATAKIWA KU...

TAASISI YA UTAFITI YATAKIWA KUISHIRIKISHA SERIKALI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ameitaka Taasisi inayojishughulisha na utafiti ya (Natural Resource Governance Institute) kuishirikisha Serikali kwenye tafiti zinazohusu Serikali ili kuwa na usahihi wa takwimu zinazotolewa.

Ameyasema hayo, Oktoba 29,2021 wakati wa kikao cha Wizara ya Nishati na Taasisi hiyo kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo katika mji wa Serikali, jijini Dodoma ambapo Taasisi hiyo iliwasilisha tafiti yao kuhusiana na rasilimali ya Gesi Asilia nchini Tanzania.

Aidha, alisema ushirikiano wa Serikali na Taasisi hizo utasaidia kupata takwimu zilizo sahihi ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa Taifa kiujumla.

“Haipendeza tafiti mbalimbali kusambazwa kwa wananchi bila ya Serikali kushirikishwa na kutoa maoni yao unapofanya tafiti lazima ungalie na upande wa pili ambao ni Serikali,” alisisitiza Mahimbali.

Alisema, Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na Taasisi hiyo katika tafiti mbalimbali na kwakuwa inaisadia Serikali kupata takwimu mbalimbali muhimu.

Kikao hicho, kilihudhiriwa na Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mohamed Fakihi, Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishegoma, Mkurugenzi wa Sera Mipango Petro Lyatuu pamoja na watumishi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizopo chini yake.