WANAFUNZI NA WAZAZI TULIWAITA… NA WAMEITIKA!
Banda la Wizara ya Nishati linaendelea kupokea watoto na wazazi wanaofika kujifunza, kuburudika na kupata uzoefu wa kipekee kuhusu sekta ya nishati.
Nawe mlete mwanao apate elimu kuhusu nishati kwa njia rahisi na ya kuvutia, aondoke na zawadi yake, pamoja na kupata huduma kutoka kwa wataalamu wetu.
Karibu Banda la Wizara ya Nishati, lililopo karibu na jengo la TANESCO katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Tunakusubiri tukuhudumie, tukuelimishe na kukupa uzoefu wa kipekee katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).