Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

Waziri Makamba akutana na ADNO...

Waziri Makamba akutana na ADNOC

Waziri Makamba akutana na ADNOC

Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu

Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Abu Dhabi (ADNOC). Waziri Makamba amefanya kikao hicho tarehe 25 Oktoba 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa ADNOC Global Trading Ltd, Ndg. Ahmed Bin Thalith ambapo walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na Abu Dhabi katika sekta ya mafuta na gesi.

Waziri Makamba pia alipata nafasi ya kutembelea ofisi za ADNOC na kujionea matumizi ya hali ya juu ya teknolojia katika kuendesha na kusimamia biashara ya mafuta.

“Tanzania tuna nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwa wenzetu kama Abu Dhabi ambao wamekuwepo katika sekta ya mafuta na gesi kwa muda mrefu na ziara hii ni sehemu ya kujifunza huko” alisema Waziri Makamba.

Waziri Makamba aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini UAE Balozi Mohamed Mtonga, Kamishna wa Petroli na Gesi kutoka Wizara ya Nishati Tanzania, Michael Mjinja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.