Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​WAZIRI MAKAMBA AWASILISHA UJU...

​WAZIRI MAKAMBA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU.

WAZIRI MAKAMBA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU.

__Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu_

Waziri wa Nishati, January Makamba, amewasilisha Ujumbe Maalum wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

WaziriMakamba amewasilisha ujumbe huo maalum kupitia kwa Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, Waziri wa Nchi anayeshughulikia mambo ya nje, tarehe 24 Oktoba, 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya UAE.

Mheshimiwa Makamba yupo Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Mafuta na Gesi

Mheshimiwa Makamba katika mazungumzo hayo ameambatana na Mhe. Mohamed Mtonga, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Kamishina wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio.