The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA UJ...

WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu (Februari 16, 2026) amekagua mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani mkoani Tanga na amesema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wake.

Amesema kuwa mradi huo ni wa kimkakati ambao utagharimu Dola za Marekani bilioni 5.65 ni kielelezo cha undugu kati ya Tanzania na Uganda. “Ninatambua msisitizo uliowekwa na viongozi wetu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Miseveni katika utekelezaji wa mradi huu.”

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ambaye yuko mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka uzito unaostahili katika kutekeleza mradi huo ambao umefikia asilimia 81 ya utekelezaji kwa heshima ya undugu kati ya Tanzania na Uganda.

“Lakini tutaendelea kuweka uzito unaostahili kwa heshima ya kulinda uhuru wetu kwa kuwa ni nchi huru ambayo inaweza kujitegemea kutekeleza mradi wa kiwango hiki, hiki ni kielelezo kwamba nchi yetu inaweza kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na miradi mikubwa ya maendeleo.” Amesema

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewatahadharisha watu wanaoanzisha makampuni na kuyaita ya wazawa huku yakiwa yanamilikiwa na wageni ili kunufaika na fursa ya ‘Local Content’ ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika mradi na kwamba watakaogundulika watafungiwa na hawatafanya kazi tena nchini.

“Wapo wasio waaminifu wanawatumia Watanzania kuanzisha makampuni wanasema ni ya wazawa. Tunataka kuinua kampuni za Watanzania, upo mchezo mgeni anatumia anuani ya Mtanzania ambaye si mnufaika, wale watakaogundulika wanafanya ujanja tutawafungia na hawatafanya kazi tena kwetu.”

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuwatapeli Watanzania na kuwaibia fursa. “Tumekupa mradi una nafasi yako tena asilimia kubwa, tunataka hiyo sehemu ndogo inawanufaishe Watanzania na ninyi mnawaibia, wale tuliowapa kazi ya kufuatilia hili tukigundua upo huu mchezo tutakuchukulia hatua kwa kuwa tutajua na wewe ni sehemu yao.” Amesema Mheshimiwa Dkt. Nchemba

Kadhalika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameagiza wasimamizi wa mradi huo wahakikishe kuwa baada ya ujenzi huo kukamilika kipaumbele cha ajira kitolewe kwa wale waliofanya kazi kwenye mradi huo kwa kuwa wanakidhi vigezo.

[16:05, 2/16/2026] Triza Madam Theresia (Teddy) Wizara: Hii imetoka ofisi ya Waziri Mkuu

[18:26, 2/16/2026] Triza Madam Theresia (Teddy) Wizara: ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 70 ZIMEKUSANYWA KUPITIA MRADI WA EACOP- MHE.SALOME

Serikali imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 70 kupitia tozo, ada na ushuru mbalimbali zitokanazo na utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), na inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 2.3 mradi utakapoanza kuingia katika hatua ya uendeshaji.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema hayo tarehe 16 Februari 2026 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika mradi wa EACOP mkoani Tanga.

Mhe. Salome amesema mradi huo ambao umefikia asilimia 81 ulianza kutekelezwa mwaka 2022 na unahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilomita 1,443 pamoja na miundombinu mingine ikiwemo matenki na gati la kupakia mafuta.

Amefafanua kuwa mradi unatekelezwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 5.649, huku Serikali ya Tanzania ikichangia dola milioni 374 sawa na asilimia 15 ya hisa.

Katika sekta ya ajira, amesema mradi umezalisha jumla ya ajira 10,000 katika kipindi cha ujenzi, ambapo asilimia 75 sawa na ajira 7,500 zimenufaisha Watanzania wenye ujuzi wa chini na kati, huku asilimia 25 sawa na ajira 2,500 zikinufaisha Watanzania katika nyanja mbalimbali za uhandisi, ujenzi wa mitambo ya umeme, mazingira n.k

Mhe. Salome ameongeza kuwa zaidi ya kampuni 200 za Kitanzania zimepata zabuni za kutoa huduma na bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.325, huku barabara zenye urefu wa kilomita 304 zikiboreshwa ili kurahisisha shughuli za ujenzi na kuchochea uchumi wa wananchi.

Mhe.Salome amemshukuru, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kutekeleza mradi huo ambapo jitihada mbalimbali anazofanya zitawezesha mradi huo kukamilika julai 2026