WAZIRI NDEJEMBI AKUTANA NA VIONGOZI WA KAMPUNI ZA SHELL NA EQUINOR KUHARAKISHA MRADI WA GESI KUSINI.
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shell Exploration and Production Tanzania Ltd pamoja na Equinor Tanzania kujadili utekelezaji na uendelezaji wa Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) katika mikoa ya kusini.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Aprili 28, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Mhe. Ndejembi alikutana na ujumbe wa Shell ulioongozwa na Makamu wa Rais anayeshughulika na ukuaji wa LNG, Kelli How, pamoja na ujumbe wa Equinor ulioongozwa na Hilde Marete.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Mussa Makame, pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani.