The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WAZIRI NDEJEMBI AWASILI TANGA...

WAZIRI NDEJEMBI AWASILI TANGA KWA ZIARA YA KIKAZI.

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb.), amewasili mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, Juni 29, 2026.

Akiwa mkoani Tanga, Waziri Ndejembi alitembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwemo Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika eneo la Chongoleani, Tanga, unaolenga kusafirisha mafuta ghafi yaliyogunduliwa nchini Uganda kwenda kwenye masoko ya kimataifa.

Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi aliambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.