WAZIRI NDEJEMBI AZINDUA KITUO CHA KUCHAJIA VYOMBO VYA USAFIRI VYA UMEME – DODOMA.
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb.), akiwa pamoja na viongozi wengine, akikata utepe na kuweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa Kituo cha Kuchajia Vyombo vya Usafiri Vinavyotumia Umeme katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) jijini Dodoma, leo tarehe 11 Juni, 2026.
Uzinduzi huo unaambatana na utiaji saini na uzinduzi wa miradi ya nishati safi, ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Kuchajia Vyombo vya Usafiri Vinavyotumia Umeme (EV Charging Stations) pamoja na Mpango wa Ukopeshaji wa Majiko ya Umeme kwa Wateja wa TANESCO (On-Bill Financing – OBF), uliofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, Jamatini jijini Dodoma.
Mradi huu unalenga kuboresha maisha ya wananchi na wateja wa TANESCO kupitia upatikanaji wa nishati safi ya umeme, nafuu na yenye ufanisi katika sekta za usafirishaji na matumizi ya kupikia.