WAZIRI WA ULINZI ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho ametembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika Banda la Wizara amepata maelezo kuhusu Sera ya Nishati ya Mwaka 2015 pamoja na mikakati mingine inayosimamiwa na Wizara ya Nishati ukiwemo Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Mkakati wa Matumizi Bora ya Nishati na Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia.