WIZARA YA NISHATI YABAINISHA MCHANGO WA NISHATI KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Wizara ya Nishati, Bw. Emilian Nyanda, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Juni 05, 2026 jijini Dodoma, ameeleza majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu nchini.
Katika wasilisho lake, Bw. Nyanda amebainisha mchango wa sekta ya nishati katika kuhifadhi mazingira kupitia matumizi ya nishati safi, gesi asilia, nishati jadidifu pamoja na teknolojia mbalimbali za nishati rafiki kwa mazingira.
Amesema juhudi hizo zinalenga kupunguza matumizi ya nishati zisizo safi, kuboresha afya ya jamii na kuchangia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, huku zikihakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.