ZAWADI KWA WANAFUNZI NA WAZAZI ZINAENDELEA KUTOLEWA KATIKA BANDA LA WIZARA YA NISHATI.
Usikose fursa hii! Tembelea Banda la Wizara ya Nishati na upate elimu sahihi kuhusu sekta ya nishati kupitia wataalamu wetu walio tayari kukuhudumia na kujibu maswali yako yote.
Watoto wanapata elimu kwa njia rahisi na ya kuvutia, huku wazazi wakipata taarifa kuhusu huduma, miradi na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya nishati.
Na si elimu tu… zawadi zinaendelea kutolewa kwa wanafunzi na wazazi wanaotembelea banda letu, huku kukiwa na surprise mbalimbali zinazowasubiri.
Karibu Banda la Wizara ya Nishati, lililopo karibu na jengo la TANESCO katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Njoo ujifunze, upate zawadi na uondoke ukiwa Balozi wa masuala ya nishati!