11 EAST AFRICAN PETROLEUM CONFERENCE AND EXHIBITION 14
View
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa maelekezo kwa wasambazaji wa Teknolojia ya Nishati Safi ya Kupikia kuhusu kuhakikisha Teknolojia hizo zinafika maeneo ya vijijini wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba na uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa uunganishaji umeme kwa wananchi kati ya TANESCO na CRDB, uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Kulia kwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera.
View
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera ( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba (aliyevaa suti ya kahawia) pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Nishati (wa mwisho kushoto ni Mhandisi Felichesmi Mramba, Katibu Mkuu Umeme na Nishati Jadidifu), wa mwisho kulia ni Dkt. James Mataragio Katibu Mkuu Mafuta na Gesi, Mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma.
View
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba (Kushoto mwa Waziri), Makatibu wakuu wa Nishati, Kamishna Wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati, wakati wa mapokezi ya Waziri alipowasili katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.
View
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera (katikati), Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba (kushoto mwa Waziri), Makatibu Wakuu, Makamishna pamoja na Viongozi wa Idara na Vitengo mbalimbali ndani ya Wizara ya Nishati wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Mapokezi ya Mhe. Waziri wa Nishati alipowasili Wizarani Mtumba Jijini Dodoma.
View
Waziri wa Nishati ,Mhe. Dkt. Juma Homera akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, wakati alipowasili rasimi katika Wizara ya Nishati.
View
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amewataka viongozi na watumishi wa Wizara ya Nishati kuongeza kasi na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora kupitia sekta ya nishati.
View
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia wa Wizara ya Nishati, Bw. Nolasco Mlay mara baada ya kuhutubia Kikao cha 81 chaBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), kinachofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York nchini Marekani, wakati akimwakilisha Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. SamiaSuluhu Hassan.
View
Viongozi mbalimbali wameungana na Rais Samia katika uzinduzi huo, akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Moustafa Madbouly; Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi; pamoja na viongozi wengine.
View
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, Agosti 22, 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, mkoani Pwani
View
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na viongozi wengine, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 katika eneo la Rufiji, mkoani Pwani, Agosti 22, 2026.
View
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba akipika kwa Nishati safi ya Kupikia (Kuni Poa) alipomtembelea Bi. Afua Juma maarufu kama Mama Manyema, kukambidhi mfumo wa Nishati safi ya kupikia katika eneo lake la kazi Mabibo Jijini Dar es Salaam.
View
The Crude Oil will be exported via a 2 km long jetty where Tankers can safely be moored and access with sufficient water depth.
View
Mradi wa umeme jua wa Kishapu mkoani Shinyanga utakaozalisha megawati 150. Kwa sasa mradi umeanza kuzalisha megawati 50 ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi.
View
Mradi wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere umejengwa katika maporomoko ya mto Rufiji umekamilika na una uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 2,115.