RECENTLY 26
View
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi akipata maelezo kuhusu mfumo wa Kidigitali wa Kupanga na kusimamia miradi ya REA (REA Digital Platform) wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika kuanzia 20 - 23 Aprili 2026 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Felchesmi Mramba na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy
View
Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mpomvu mkoani Geita, chenye uwezo wa megawati 90.
Kituo kimeimarisha hali ya umeme katika Mikoa ya Geita, Kagera, Mwanza na Kigoma.
View
Deputy Minister for Energy Hon. Salome Makamba switching on electricity in Mdyandelema Hamlet, Uvinza District, Kigoma Region, during her visit to the 49.5 MW Malagarasi Hydropower project. Mdyandelema is among the 18 hamlets electrified through the project.
View
Mahumbika power substation in Lindi region with 35MVA capacity
View
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga ambao chenye uwezo wa 2X60MVA 132/33kV, pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi
View
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameshiriki Mdahalo wa Ngazi ya Juu wa Mawaziri ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) jijini Paris, ambapo ameeleza kuhusu mafanikio yanayoendelea kupatikana Tanzania katika nishati safi ya kupikia.
View
Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba (Mb.), akipika kwa nishati
safi ya kupikia mara baada ya kuzindua mradi huo katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Kondoa Mkoani Dodoma leo tarehe 17.02.2026.
View
Picha ya pamoja ya viongozi kutoka nchi mbalimbali duniani katika Maadhimisho ya Wiki ya Nishati yaliyo adhimishwa katika Jimbo la Goa’ nchini India kuanzia tarehe 27-30 January 2026.
View
Waziri wa NishatiMhe, Deogratius Ndejembi azindua Mita janja katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na watendaji wa TANESCO, Disemba 05, 2025.
View
Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb), akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla wa uapisho wa mawaziri iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma
View
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome W. Makamba (Mb), akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya uapisho wa mawaziri iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma.
View
Baadhi ya mabomba yatakayotumika kwenye mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP).
View
Muonekano wa jengo la Wizara ya Nishati baada ya kukamilika kwake katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma
View
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio (kulia) akipokea maua mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma tarehe 11 Machi, 2024.
View
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (wa Nne kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na viongozi waandamizi kutoka Wizara zinazohusika na Sekta ya Nishati mara baada ya kikao chao katika Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wanaohusika na mfumo wa pamoja wa umeme kwa nchi za Mashariki ya Afrika (EAPP Council of Ministers) ambao unafanyika kwa siku mbili jijini Nairobi nchi Kenya.
View
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria uwashaji umeme katika Kijiji cha Ikwavila wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka na wa tatu kutoka kulia Mbunge wa Wanging’ombe Dkt.Festo Dugange.
View
Mitambo ya kuchoronga visima vya uhakiki (drilling rig) kwa miradi ya Jotoardhi nchini ikiwa imefungwa katika chanzo cha Jotoardhi cha Ngozi (70MW) wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
View
Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya, mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi mkoani humo.
View
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 49.5 kwa nguvu ya maji katika Mto Malagarasi mkoani Kigoma. Wanaosaini ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (kulia) na Meneja Mradi kutoka kampuni ya Dongfang Electric International ya nchini China, Ni Zhihong. Hafla ya utiaji saini imefanyika jijini Dodoma, tarehe 08 Februari, 2024.
View
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na watendaji mbalimbali wa Serikali na kampuni ya EACOP kabla kukagua kazi mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mafuta ghafi kutoka Uganda katika kata ya Chongoleani jijini Tanga. Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba
View
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Nyumba, Nishati na Maendeleo ya Makazi wa nchi hiyo, Mhe. Assem Elgazzar katika kikao kilicholenga maendeleo ya mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) kilichofanyika jijini leo Disemba 21, 2023 Dar es Salaam
View
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (katikati) akitembelea na kukagua Miundombinu ya Upakuaji wa Mafuta ya aina yote yanayoingia
na kutoka nchini wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala huo, Tarehe 09 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam
View
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko
akitambulisha viongozi mbalimbali waliofika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kumpokea Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu
Guozhong ambaye amewasili nchini kwa ziara ya siku Tatu.
View
Nguzo zikiwa zimepangwa na nyingine kutandazwa chini zikisubiri kukauka kwa kutumia miale ya jua katika moja ya viwanda vya nguzo mkoani Iringa.
View
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiangalia sehemu ya ujenzi wa mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ambapo alizindua tukio la uchepushaji wa maji ya mto Rufiji kwenye handaki ili kupisha ujenzi wa tuta kuu la bwawa la kufua umeme mkoani Pwani, Novemba 18, 2020.