Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

TANGAZO LA FURSA YA MKOPO NAFU...

TANGAZO LA FURSA YA MKOPO NAFUU - UJENZI NA UENDESHAJI WA VITUO VIDOGO VYA MAFUTA MAENEO YA VIJIJINI

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imedhamiria kuanzisha mpango wa kuwezesha ujenzi wa vituo vipya vidogo vya mafuta (petroli na dizeli) vya gharama nafuu maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yatokanayo na njia zisizo salama.

Wakala unakaribisha waomabaji wenye vigezo kuomba mkopo ili kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini. Fomu ya Maombi pamoja na Mwongozo wa Maombi ya Mkopo vimeambatanishwa kwenye tangazo hili kwenye tovuti ya Wakala.

Maombi yote yawasilishwe kupitia barua pepe: vituovyamafuta@rea.go.tz na pia kupitia anuani ifuatayo:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini – REA
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania.

Juu ya bahasha baada ya anuani ya Wakala iandikwe ‘Maombi ya Mkopo kwa Ajili ya Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini’

Mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo ni tarehe 25/8/2023 saa tisa na nusu alasiri.

https://rea.go.tz/Articles/maombi-ya-mkopo-wa-ujenzi-na-uendeshaji-vituo-vidogo-vya-mafuta-vijijini-petroli-na-dizeli