Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​ALIYOZUNGUMZA NAIBU WAZIRI WA...

​ALIYOZUNGUMZA NAIBU WAZIRI WA NISHATI, STEPHEN BYABATO KATIKA HAFLA YA MAKABIDHIANO YA LESENI YA UCHIMBAJI MKUBWA KWA KAMPUNI YA TEMBO NICKEL CORPORATION LTD NA UZINDUZI WA TAARIFA YA UHAMAS

ALIYOZUNGUMZA NAIBU WAZIRI WA NISHATI, STEPHEN BYABATO KATIKA HAFLA YA MAKABIDHIANO YA LESENI YA UCHIMBAJI MKUBWA KWA KAMPUNI YA TEMBO NICKEL CORPORATION LTD NA UZINDUZI WA TAARIFA YA UHAMASISHAJI UWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA SEKTA YA MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, Steven Byabato

  • vTutamfikishia mteja umeme ili aweze kufanya shughuli zake mara atakapokuwa tayari.

vNampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuifanya Tanzania kuwa mjumbe wa TEITI inayowafanya wenye utajiri wa rasilimali madini, mafuta na gesi kushirikiana katika kuona mataifa yao yananufaika na uwepo wa rasilimali hizo.

vTanzania imeenda mbele zaidi ya kuandaa sheria mwaka 2015 yenye kanuni za mwaka 2019 na kufanyiwa marejeo mwaka 2021 yenye lengo la kusimamia tasnia muhimu ya uziduaji.

vSheria hiyo inayataka makampuni ya madini, mafuta na gesi kutoa taarifa ili kuiwezesha Serikali kujua umelipa kodi kiasi gani na umeyalipa kiasi gani makampuni binafsi yanayotoa huduma katika mgodi wako ili kuwa na uzani unaofanana

vFaini ya kutokutoa taarifa hizo kwa makampuni yaliyowekeza kwenye tasnia ya uziduaji ni shilingi milioni 100 hii ni kuonesha kuwa serikali imedhamiria kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha sekta binafsi na serikali kukaa pamoja na kujadiliana kuona mapato yanayotokana na rasilimali za mafuta, gesi na madini yanatumika katika uendelezaji wa eneo letu katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

vWizara ya Nishati ni walengwa katika jambo hili, tunachimba gesi lakini pia Gesi Asilia kwa sasa inachangia asilimia 60 katika uzalishaji umeme na sasa tumejiandaa kuanza utekelezaji wa mradi wa LNG kutoka Lindi ambapo kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 30 zitatumika kwenye mradi huo.

vWizara ya Nishati tupo tayari kutoa ushirikiano na kusimamia sheria kwani tunao wajibu kwenye eneo hili.

vKutolewa kwa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ni fusra kwa Wizara ya Nishati kwani tunapata mteja mpya kutokana na mahitaji ya umeme katika uendeshaji wa shughuli za mgodi.

vTuna taarifa kuwa mgodi utakapoanza utahitaji megawati 8, Mkoa wa Kagera kwa sasa unatumia takribani megawati 17 Serikali imejipanga kuhakikisha gridi ya Taifa inafika Mkoa wa Kagera mapema iwezekanavyo na kukamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Nyakanazi na mradi wa uzalishaji umeme wa Rusumo.

vTukikamilisha mradi wa Julius Nyerere, tukapata megawati 2115, tukakamilisha mradi wa Rusumo na kupata megawati 27 tutakuwa na umeme mwingi sana na hivyo niwahakikishie wawekezaji na wawekezaji wengine wanaotaka kuja kuwekeza Tanzania na tunaahidi kila atakayehitaji umeme atapata huduma hiyo.