Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana
Baaraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati limefanya mkutano wa dharura ili kujadili rasimu ya miundo ya maendeleo ya utumishi kwa kada zilizo chini ya Wizara ya Nishati.
Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na kufanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba-Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, Viongozi wa TUGHE Taifa, Mkoa na Tawi la Nishati, Mwakilishi wa Kamishna wa Kazi, Menejimenti ya Wizara ya Nishati, Wawakilishi wa Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati.