Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

BYABATO ASHIRIKI MKUTANO WA 16...

BYABATO ASHIRIKI MKUTANO WA 16 WA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA EAPP

BYABATO ASHIRIKI MKUTANO WA 16 WA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA EAPP

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameshiriki Mkutano wa 16 wa Mawaziri wanaohusika na Umeme kutoka nchi za Mashariki mwa Afrika ambazo zimeunganisha mifumo ya kusafirisha umeme baina yake (Eastern Africa Power Pool – EAPP).

Mkutano hup ulijadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya kuunganisha Gridi za umeme, Mkataba wa makubaliano ya awali kuhusu wajibu wa masuala mbalimbali ya ushirikiano na Uteuzi wa Katibu Mtendaji.katika nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool – EAPP uliofanyika nchini Uganda jana tarehe 03 Februari 2023.

Naibu Waziri Byabato katika mkutano huo aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha.Modestus Lumato.