Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

DKT. BITEKO AHIMIZA WATANZANIA...

DKT. BITEKO AHIMIZA WATANZANIA KUPIGA KURA NOVEMBA 27, 2024

Asisitiza Kupiga Kura ni Haki ya Kikatiba

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto BitekoamewahimizaWatanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo leo Novemba 25, 2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia nchini.

“Naomba Watanzania wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaakatika maeneo yao wajitokeze kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wao,” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “ Viongozi hawa ndio msingi katika nchi yetu, viongozi hawa ndio wanajua watu wanaishije, wana shida gani na watafanya nini kutatua shida hizo. Ni muhimu wote kushiriki kuchagua viongozi tunaowataka,” amesisitiza.

Aidha, Dkt. Biteko amebainisha kuwa kupiga kura ni haki ya kilaMtanzania mwenye sifa hivyo watu wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura ifikapo Novemba 27, 2024.