Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

DKT.DOTO BITEKO AENDELEA NA MC...

DKT.DOTO BITEKO AENDELEA NA MCHAKAMCHAKA WA KUWASHA UMEME VIJIJINI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko ameendelea na ziara yake ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini ambayo imejumuisha kuwasha umemekatika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Biharamulo, na leo amewasha umeme katika kijiji cha Ntanga na Kasharazi wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na wanachi katika kijiji cha Ntanga na Kasharazi, amesema kuwa, Wilayaya Ngara ina vijiji 75 ambapo mpaka sasa vijiji 43 tayari vina umeme na kwa vijiji ambavyo bado havina umeme, amewaagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa, vijiji hivyo vinapelekewa umeme na baadaye kuanza mpango wa kupeleka umeme kwenye vitongoji.

Amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini mkoani Kagera ikiwemo wilaya ya Ngara hivyo amewaahidi wananchi kuwa umeme utafika kwenye maeneo yote.

Katika hatua nyingine, Dkt.Biteko ameagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wakandarasi wa umeme kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele cha matumizi ya vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi ikiwemo nguzo, mita na transfoma.

“Nchi hii tulihamasisha ujenzi wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya umeme, lakini muda mwingi utaona tunajishughulisha na kununua vifaa nje ya nchi, tunatumia Dola nyingi kuagiza vifaa vya umeme wakati tuna viwanda vipo ndani, natamani mjengee uwezo viwanda vyetu vya ndani ili viweze kuzalisha zaidi na hivyo tukuze uchumi wa watu wetu.”amesema Dkt. Biteko

Amesema kuwa, viwanda hivyo vimejengwa ili viweze kusambaza vifaa kwa TANESCO, REA na wakandarasi wa umeme hivyo si sahihi kwa vifaa hivyo kuagizwa kutoka nje ya nchi.