Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

DKT.KAZUNGU AFANYA MAZUNGUMZO...

DKT.KAZUNGU AFANYA MAZUNGUMZO NA WAJUMBE KUTOKA SHIRIKA LA MAENDELEO LA SAUDIA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Khatibu Kazungu amekutana na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Saudia(Saud Fund for International Development (SFD) na kufanya mazungumzo kuhusuutekelezaji wamradi wanjia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Benaco wilayani Ngara hadi Kyaka wilayani Misenyipamoja na kituo cha kupooza umeme cha Benaco mkoani Kagera.

Kikao kazi hicho kimefanyika jijini Dodoma, Februari 19, 2025.

Dkt. Kazungu ameishukuru SFD kwa ufadhili wake katika miradi mbalimbali nchini ikiwemo miradi ya Nishati na kuahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana nao katika kufanikisha miradi hiyo ukiwemo mradi wa Benaco - Kyaka ambao unafadhiliwa kwa ushirikiano baina ya SFD, OPEC na ADFD. Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Ujumbe wa SFD uliongozwa na Ahmed Al Misfer ambaye ni Msimamizi wa Miradi katika shirika hilo