DKT. MATARAGIO AKUTANA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA CNOOC KUTOKA CHINA
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta Dkt. James Mataragio amekutana na kufanya mazungumzo na kampuni ya uwekezaji ya inayojihusisha masuala ya mafuta na Gesi kutoka China( CNOOC) kujadili maendeleo ya ushiriki wa kampuni hiyo katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), pamoja na fursa nyingine za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini. Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es as salaam, Semtemba 18, 2026,Dkt. Mataragio amesema Tanzania inafursa nyingi za uwekezaji katika miradi mbalimbali ya Sekta za Nishati husasani katika mafuta na gesi. Katika kikao hicho Dkt. Mataragio amezungumzia mkoa wa Tanga kuwa unatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha nishati nchini, kutokana na mipango mbalimbali ya kuendeleza miundombinu ya nishati, ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta,bomba la gesi pamoja na bomba la bidhaa nyeupe linalotarajiwa kuwa na uwezo wa kusafirisha bidhaa katika pande zote mbili kati ya Uganda na Tanzania. aidha ameipongeza kampuni ya CNOOC kwa ushiriki katika Mradi wa EACOP na kueleza kuwa mradi huo ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali, ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 92, huku mafuta ya kwanza yakitarajiwa kupatikana mwezi Desemba mwaka huu. Kikao hicho kimehushiriwa na Kamishna wa Petroli Wizara ya Nishati, Godluck Shirima na Wataalam wengine kutoka Wizara ya Nishati. Kwa upande wake mwakilishi kutoka kampuni ya CNOOC, ilieleza nia ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi, hususan utafutaji wa mafuta na gesi baharini (offshore), na nia ya kushiriki katika Duru ya 5 ya kunadi vitalu. Aidha, CNOOC ilieleza nia ya kushiriki katika Mradi wa LNG na kuimarisha ushirikiano na shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na wadau wengine katika sekta ya nishati. Kampuni hiyo pia ilihimizwa kuendelea kuwasilisha kwa Serikali maeneo mengine ambayo ina nia ya kuwekeza ili kuwezesha majadiliano na ushirikiano zaidi.