Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

DKT. MATARAGIO: MRADI WA TAZA...

DKT. MATARAGIO: MRADI WA TAZA NI UTEKELEZAJI WA MPANGO MAHSUSI WA NISHATI (MISSION 300)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt.James Mataragio amesema kuwa utekelezaji wa Mradi wa TAZA unachangia kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa Mpango Mahususi wa Nishati (MISSION 300) uliokubaliwa katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika.

Pia umekua chanzo kikubwa cha maendeleo katika Sekta ya Nishati Tanzania na miradi mingine ya maendeleo nchini.

Dkt. Mataragio ameyasema haya tarehe 15 Septemba 2025, wakati wa kikao cha Wadau na wawezeshaji wa utekelezaji wa mradi wa TAZA (Implementation Support Mission) katika Ofisi za Wizara ya Nishati Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza Kuwa mpango wa Serikali ya Tanzania ni kuanzisha miradi ya kuzalisha Umeme itakayounganisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Nchi ya Demokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na Malawi.

Dkt. Matarajio ameendelea kusisitiza kuwa Mradi huo ni Muhimu kwa nchi yetu kwakuwa utekelezaji wake utaiwekaTanzania katika nafasi Kubwa zaidi Katika utekelezaji wa Miradi ya Umeme.

Amefafanua kuwa mradi wa TAZA utaongeza nguvu na uwezo wa kusafirisha umeme nchini kupitia Iringa-Kisada-Mbeya-Tunduma-Sumbawanga na kufikia 1,700MV umeme ambao utakao safirishwa.

Aidha, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inatekeleza mradi wa TAZA (Tanzania-Zambia Transimission Interconnection Project) ambao utaunganisha Umeme kupitia Gridi za Taifa nchini Tanzania na nchi jirani ya Zambia.

Amewashukuru wawezeshaji hao kwa kuendelea kuwekeza nchini na kudumisha mashirikiano katika sekta ya Nishati Tanzania kwakuwa kumekuwa na mchango mkubwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini.

Kikao hicho kiliwashirikisha Wadau wanao wezesha utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na kuwezeshwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (International Development Association (IDA), Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Ufarans (AFD), na Umoja wa Ulaya (EU).

Kwa upande wa Mtaalamu wa Nishati kutoka Benki ya Dunia Dkt. Rhonda Jordan Antoine amesema kuwa " Benki ya Dunia inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuwezesha upatikanaji wa fedha za miradi ambayo ni kichocheo cha maendeleo katika jamii na hatua mojawapo ya utekelezaji wa mpango mahususi wa Nishati- Mission 300."

Dkt. Antoine amefafanua zaidi kuwa Mradi wa TAZA unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme umbali wa jumla ya kilometa 616 pamoja na vituo vya kupoza umeme katika mikoa ya Iringa-(Kisada) Kilometa 106, Mbeya Kilometa 185, Mbeya -(Tunduma) Kilometa 122 pamoja na1 mradi wa kusafirisha Umeme Rukwa - (Simbawanga) wenye urefu wa kilometa 203.