The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

JUKWAA LA SIKU YA NISHATI LAWA...

JUKWAA LA SIKU YA NISHATI LAWAKUTANISHA VIONGOZI NA WADAU SABASABA.

Wadau mbalimbali wamewasili katika Ukumbi wa Mwandoro, uliopo Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, kushiriki Kongamano la Siku ya Nishati.

Jukwaa hili muhimu limewakutanisha viongozi, watunga sera, wataalam, wawekezaji, washirika wa maendeleo na wadau wa sekta ya nishati kujadili mwelekeo wa sekta, fursa za uwekezaji, ubunifu na teknolojia, pamoja na mchango wa sekta ya nishati katika kukuza uchumi wa Taifa.

Washiriki wanatarajiwa kufuatilia mawasilisho ya kitaalamu na kushiriki katika majadiliano ya kimkakati yatakayojikita katika kuimarisha upatikanaji wa nishati ya uhakika na endelevu, kuhamasisha uwekezaji, kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia, na kuharakisha utekelezaji wa azma ya Serikali ya kufikia uzalishaji wa megawati 8,000 za umeme ifikapo mwaka 2030.