The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA...

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATAKA MIRADI YA LNG NA CNG KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA TAIFA NA WAZAWA.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mhe. Simon Songe imepokea na kujadili taarifa ya Maendeleo ya Miradi ya Gesi Asilia ya LNG na CNG ambapo imeelekeza Wizara ya Nishati kuhakikisha miradi hiyo inaleta manufaa kwa Taifa pamoja na kuwanufaisha wazawa kupitia shughuli za uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Taarifa ya miradi hiyo imewasilishwa mbele ya kamati hiyo na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi Agosti 18, 2026 katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imeeleza maendeleo ya Mradi wa Tanzania LNG fursa ya gesi asilia katika biashara ya kimataifa, pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuongeza matumizi ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) katika usafirishaji na maeneo mbalimbali nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati.