Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imekutana na Viongozi watendaji Wizara ya Nishati
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Subira Mgalu (Mb), imekutana na viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati pamoja na baadhi ya taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Lengo la kikao hicho ni kupata uelewa wa kina kuhusu muundo na majukumu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kikao hicho kimefanyika leo, Januari 21, 2025, katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.