The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA N...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI IMEPOKEA TAARIFA KUHUSU SERA, SHERIA NA MUUNDO WA MAJUKUMU YA WIZARA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe.Subira Mgalu imepokea taarifa kuhusu Sera, Sheria, Muundo na Majukumu ya Wizara ya Nishati katika kikao cha kwanza kati ya Kamati hiyo na viongozi wa Wizara ya Nishati pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.Kikao hicho kimefanyikaleo Januari 20,2026 kwenye kumbi za Bunge jijini Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi,Naibu Waziri Nishati, Mhe. Salome Makamba na Katibu Mkuu Mha. Felichesm Mramba.