Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​MAENEO YENYE UZALISHAJI YAPEW...

​MAENEO YENYE UZALISHAJI YAPEWE KIPAUMBELE CHA UMEME-BYABATO

MAENEO YENYE UZALISHAJI YAPEWE KIPAUMBELE CHA UMEME-BYABATO

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuyapatia kipaumbele cha umeme maeneo yenye shughuli za uzalishaji ili kutoathiri shughuli zao.

Byabato alitoa agizo hilo Novemba 23,2022 akiwa jijini Arusha, wakati akizungumza na wananchi kwenye ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuwa, ili kuweza kuyabaini maeneo yote yenye shughuli za uzalishaji, TANESCO washirikiane na Mamlaka za Serikali za Mitaa na baada ya kubaini maeneo hayo wayapatie kipaumbele katika kipindi hiki.

Alieleza kuwa, katika umeme unaozalishwa nchini, asilimia 60 hadi 70, unatokana na chanzo cha Gesi Asilia na asilimia 30 unatokana na maji.


Aliongeza kuwa, mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakapokamilika utaondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini kwani jumla ya megawati 2115 zinategemewa kuzalishwa kutokana na mradi huo wa JNHPP.