Makatibu Wakuu wapitia maboresho ya rasimu Nishati Safi ya Kupikia
Makatibu Wakuu wapitia maboresho ya rasimu Nishati Safi ya Kupikia
Kikao cha Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu wamekutana kupitia maboresho yaliyofanywa katika rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033.
Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi kilichofanyika Aprili 9 mkoani Dodoma kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Kikao hicho kimehusisha Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya wataalam wa nishati safi ya kupikia, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga na Wajumbe wa Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia.
Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa kikao kama hicho kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijini Dodoma mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa maboresho na maelekezo yaliotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokutana na Mawaziri na NaibuMawaziri Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.
Mara baada ya Makatibu Wakuu hao kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi safi ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 na Rasimu ya Mpango Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, rasimu hizo zitawasilishwa kwa Waziri Mkuu na kujadiliwa katika kikao kitakachojumuisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, Timu ya Wataalam na wadau wa sekta ya nishati safi ya kupikia kitakachofanyika tarehe 17 Mei 2023.