MHA. MRAMBA AVUTIWA NA KASI YA REA KUSAMBAZA UMEME KWENYE VITONGOJI.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu) Mha. Felchesmi Mramba ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na mafanikio ya usambazaji umeme kwenye vitongoji.
Mha. Mramba amesema hayo Julai 13, 2026 alipotembelea banda la REA kwenye Kilele cha maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).