Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

MHANDISI MRAMBA ASHIRIKI MKUTA...

MHANDISI MRAMBA ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA NGUVU ZA ATOMIKI NCHINI AUSTRIA

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha.Felchesmi Mramba ameshiriki mkutano wa 69 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki -IAEA jijini Vienna Austria ambao unawashirikisha wadau mbalimbali wanaotumia nishati ya nyuklia kama chanzo cha umeme.

Mha. Mramba anashiriki mkutano huo wa kimataifa unaowakutanisha wadau mbalimbali na mataifa makubwa yanayotumia nyuklia kama chanzo kimojawapo cha kuzalisha umeme.

Mkutano huo unakuja kipindi ambacho Wizara ya Nishati imepewa jukumu kubwa na Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, la kuhakikiaha TANESCO inaaza kuzalisha umeme kwa kutumia madini ya Uranium yanayopatikana Namtumbo mkoa wa Ruvuma.

Tanzania inatarajia kutumia vema fursa ya mkutano huo wa 69 wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuzalisha umeme kwa nguvu ya nyuklia ,pamoja na kuangalia fursa za uwekezaji kwenye miradi ya umeme .

Ujumbe wa Tanzania unaongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo.

Wajumbe Wengine walioshiriki Mkutano huo ni pamoja na

Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu Nchini Austria, Mhe. Naimi S. H. Aziz, Mha. Joseph John Kirangi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Maji na Ardhi ya Zanzibar, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati Mha. Innocent Luoga pamoja na Viongozi Waandamizi na Wataalam kutoka Kamisheni ya Nguvu za Atomi (TAEC).