The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

MHE.NDEJEMBI ATOA SHUKRAN ZAKE...

MHE.NDEJEMBI ATOA SHUKRAN ZAKE ZA DHATI BUNGENI KWA MHE.RAIS DKT.SAMIA.

"Shukran zangu za Dhati zinaanza kwenda kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Kwa Imani aliyoionesha kwangu situ katika uteuzi huu wakuweza kuwa msaidizi wake namba moja Kama makamu wake wa Rais, Lakini imani yake aliiweka kwangu kwa kuanza kuniteua kunipeleka ofisi ya Rais Tamisemi,Kwa kuniteua kuwa Waziri waNchi Ofisi yaWaziri Mkuu kazi Vijana na Ajira na Watu wenye Ulemavu,Kwa kuniteua Kuwa Waziri wake wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mwisho kabisa kwa kuniteua kuwa Waziri wa Nishati,Niimani kubwa sana Mhe.Rais ameionesha kwangu kuweza kunipa Dhamana hii yakuwa Msaidizi wake yaani Makamu wake". Amesema Mhe.Ndejembi.

Mhe.Ndejembi ameyasema hayo leo Agosti 28,2026,Bungeni Dodoma, wakati akitokea Nchini Marekani katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Uzinduzi wa ATLAS uliofanyika Agosti 26-27, 2026 jijini Washington, D.C., Nchini Humo.