MILANGO YA UWEKEZAJI NISHATI IPO WAZI- MAKAMBA
MILANGO YA UWEKEZAJI NISHATI IPO WAZI- MAKAMBA
Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba amesema Tanzania imeweka milango wazi kwenye uwekezaji wa Sekta ya Nishati kutokana na uwepo wa mahitaji makubwa ya nishati nchini.
Waziri Makamba ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam katika mkutano wa Wadau wa Nishati, Wawekezaji, Makampuni ya Nishati kutoka Nje, Mabalozi wa Nchi mbalimbali ambao unaangazia hali ya nishati sambamba na maendeleo yaliyofikiwa.
"Tumewakaribisha wawekezaji, tupo tayari kuhakikisha uwekezaji wao unakuwa wenye tija zaidi, hata hivyo serikali ipo tayari kuweka nguvu kwa sekta binafsi kwa maslahi mapana ya kupiga hatua za kimaendeleo nchini Tanzania”. Amesisitiza
Waziri Makamba amesema “Kwanini Tanzania?, Kwanini sasa? Tanzania ni mahali sahihi penye amani katika kufanya uwekezaji, hivyo tunawakaribisha Wawekezaji wenye tija kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati Nchini”
Kwa upande wao Washiriki katika Mkutano huo wamepongeza juhudi za Serikali katika Sekta ya Nishati kwa kufungua wigo wa uwekezaji sambamba na kutatua changamoto zinazoikabili Sekta hiyo ikiwemo urasimu.
Mkutano umeandaliwa na EnergyNet kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati, EWURA, TPDC na TANESCO