MKURUGENZI MSAIDIZI TAKUKURU ATEMBELEA BANDA LA NISHATI NANENANE.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti kutokaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dkt. John Joseph, ametembelea Banda la Wizara ya Nishati katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt.John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.
Akiwa katika banda la Wizara, mkurugenzi huyo amepongeza juhudi zinazofanywa na Wizara ya Nishati katika kuwapa hamasa wananchi kutumia nishati safi ya kupikia, hamasa ambayo imepelekea matumizi ya nishati hiyo kuongezeka kutoka asilimia 6.9 ya mwaka 2021 hadi asilimia 28.6.