Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AON...

​NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AONGOZA SEMINA KWA KAMATI YA WATAALAMU WA KIKUNDI KAZI CHA TAIFA CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AONGOZA SEMINA KWA KAMATI YA WATAALAMU WA KIKUNDI KAZI CHA TAIFA CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka ameongoza Semina kwa Kamati ya Wataalam ya Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia ili kuwajengea Uwezo Katika Masuala ya biashara ya kaboni katika kuwezesha utekelezaji wa miradi ya Nishati Safi ya Kupikia Nchini.

Katika kikao hicho, Mbuttuka alisisitiza kuwa kuna fursa kubwa kwa Taifa kunufaika na biashara ya kaboni kupitia misitu ya asili iliyopo nchini pamoja na miradi mbalimbali ya Nishati Safi ya Kupikia.

Mbuttuka alielezea umuhimu wa kuwajengea uwezo wataalamu wazawa katika masuala ya biashara ya kaboni ili Taifa liwe katika nafasi nzuri ya kunufaika na wataalamu hao.

Vilevile, Mbuttuka aliwaelekeza wadau wa Nishati Safi ya Kupikia kuanza kutengeneza teknolojia zenye uwezo wa kutumika katika Taasisi kubwa na kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ili kuongeza kasi ya usambazaji wa Nishati Safi ya kupikia Nchini Tanzania.

Aidha Mkurugenzi kutoka kampuni ya UpEnergy Bi. Rehema Mbalamwezi alielezea juu ya biashara ya kaboni ilivyowawezesha kutoa ruzuku katika majiko banifu na majiko sanifu ya umeme (pressure cookers) ili wananchi waweze kumudu gharama za awali za majiko hayo.

Pia, Alielezea juu ya utumiaji wa teknolojia hizo sanifu zinavyosaidia katika utunzaji wa mazingira na kuokoa gharama za matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa watumiaji.

Naye Bw. Jafary Mashaka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Afrihands ameelezea umuhimu wa bayogesi kama moja ya teknolojia inayoweza kutumika katika taasisi kubwa kwa ajili ya kupikia na kuacha mazingira safi na salama kwa kuwa bayogesi haiachi moshi kama ilivyo kwa nishati zisizo safi, pia mabaki yanayotokana na uzalishaji wa bayogesi hutumika kuboresha rutuba ya ardhi kama mbolea safi isiyo na kemikali. Matumizi ya bayogesi na humpa mtumiaji muda wa kutosha kufanya shughuli zingine za kiuchumi.