Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe....

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, wameshiriki katika hafla fupi ya chakula cha jioni sambamba na kupata burudani (Cocktail) iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati ya Serikali ya Zimbambe.

Wengine walioshiriki ni Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.