The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

NDEJEMBI ATEMBELEA OFISI ZA UB...

NDEJEMBI ATEMBELEA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA KATIKA FALME ZA KIARABU

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo, Bw. Bakari Ameir.

Ziara hiyo imefanyika wakati wa Mkutano wa Baraza la Kimataifa la Nishati Jadidifu (IRENA) ulioanza Januari 10 na utahitimishwa Januari 15, 2026, ambapo katika ziara hiyo ameambatana na Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Mhandisi Imani Mruma, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO, TGDC na EWURA.