RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI SABASABA.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika kilele cha Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Julai 13, 2026.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Mwinyi alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, ambao walimpatia maelezo kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na Wizara ya Nishati na TANESCO kupitia maonesho hayo.