Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

RAIS SAMIA AIWEZESHA REA BILIO...

RAIS SAMIA AIWEZESHA REA BILIONI 96.8 UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI DODOMA

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 96.8 ili kuhakikisha miradi ya umeme vijijini inatekelezwa katika mkoa wa Dodoma na wananchi wanapatiwa huduma ya umeme ili kuwapatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii

Hayo yamebainishwa Aprili 12, 2025 na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 15 (HEP IIA) katika jimbo la Mvumi mkoa wa Dodoma

Mhe. Kapinga amesema, REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi ilikuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha wananchi.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Mvumi, Mhe. Livingstone Joseph Lusinde amesemaMwaka 2010 umeme ulikua kwenye vijiji viwili pekee lakini sasa vijiji vyote 60 vimefikiwa na huduma ya umeme na kuwaongezea chachu ya kufanya maendeleo wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja ameipongea REA kwa kuendelea kutekeleza miradi ya umeme vijijini ambayo imekuwa chachu ya maendeleo mkoani Dodoma.

Naye, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini Mha. Jones Olotu amesema kuwa, Mkoa wa Dodoma una jumla ya vijiji 580 ambapo vijiji vyote sawa na asilimia 100 vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya awali kama vile REA awamu ya kwanza (REA I), REA awamu ya pili (REA II), REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza (REA III Round I), na REA awamu ya tatu mzunguko wa pili (REA III Round II).

"Jumla ya vitongoji 1,773 na mitaa 225 vimefikiwa na huduma ya umeme kati ya vitongoji 3,212 na mitaa 258 ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni sawa na asilimia 57 ya vitongoji vyote, " Amesema Mha. Olotu

Mha. Olotu ameongeza kuwa, Wakala unaendelea na utekelezaji wa mradi waHEPIIA katika vitongoji 150 vya mkoa wa Dodoma kupitia mkandarasi Derm Group Ltd ambapo hadi kufikia mwezi March 2025, mkandarasi amekwisha kusimamisha nguzo katika vitongoji vyote.