Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWAS...

​RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASHA UMEME WA GRIDI KASULU, KIGOMA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASHA UMEME WA GRIDI KASULU, KIGOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu tarehe 17 Oktoba, 2022 kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, amewasha umeme wa Gridi ya Taifa katika Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma na kuzima mitambo mitatu ya mafuta yenye uwezo wa kuzalisha megawati 3.75 za umeme na kuusambaza kwenye maeneo ya Wilaya ya Kasulu na Buhigwe.

Mitambo hiyo ya mafuta ilikuwa ikigharimu gjharama kubwa kuiendesha ambapo Serikali ilikuwa ikitumia shilingi bilioni 13 kwa mwaka na matengenezo ya mitambo ya shilingi bilioni 1 kwa mwaka.

Kwa kuwasha umeme huo wa Gridi, Wilaya za Kasulu na Buhigwe zimeunganishwa na umeme wa gridi kupitia kwenye kituo kikubwa cha Nyakanazi kupitia Wilaya za Kakonko na Kibondo ambapo kwa sasa umeme unaofika mkoani humo ni wa kutosheleza mahitaji tofauti na hapo awali.

Akizungumza na wananchi, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Kigoma kuilinda na kuitunza miundombinu ya umeme iliyopita mkoani humo ili iweze kuwaletea manufaa katika shughuli zao za maendeleo.

Aidha, Rais Samia amesema kwa hivi sasa mkoa wa Kigoma utapata umeme wa moja kwa moja na wa uhakika ambao utavutia wawekezaji mkoani humo na hivyo kukuza uchumi.