Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​SHIMIWI NI MAHALA PA KAZI – B...

​SHIMIWI NI MAHALA PA KAZI – Bi ZIANA MLAWA

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Bi. Ziana Mlawa leo amesema kushiriki michezo mbali mbali inasaidia katika kujenga afya ya mwili na akili hivyo mtumishi anapopata nafasi ya kushiriki michezo yeyote aitumie ipasavyo pia husaidia hali itakayowajengea uwezo kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi.

Bi. Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Nishati watakao shiriki michezo ya SHIMIWI itakayofanyika jijini Mwanza kwanzia tarehe 1 Septemba 2025

" Pamoja na kushiriki michezo ambapo ni mbali na eneo la kazi mkumbuke mkiwa huko ni eneo la kazi nidhamu na uadilifu uwe kipau mbele mdaa wote muwapo kwenye michezo hiyo." Amesisitiza Bi. Mlawa

Ameongeza kuwa watumishi hao wajitahidi wapate ushindi ambapo kwa ushindi huo Wizara itapata heshima njee na ndani ya Wizara