Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

TAASISI 762 ZATUMIA NISHATI SA...

TAASISI 762 ZATUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NCHINI- DKT.MPANGO

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip IsdorMpango ameeleza kuwa jumla ya taasisi 762 nchini zinatumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni jitihada za kuepuka athari za kimazingira, kiafya, kijamii na kiuchumi.

Amesema hayo tarehe 5 Juni 2025 katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambayokitaifa imeadhimishwa jijini Dodoma katika kituo chaMikutano cha Jakaya Kikwete.

"Taasisi nyingi za Serikali na Binafsi zimeanza kutekeleza katazo la matumizi ya nishati isiyo safi nakuanza kutumia nishati safi ya kupikia ambapohadi Machi 2025 jumla ya Taasisi 762 zilikuwa zimeanza kutumia nishati safi ya kupikia." Amesema Dkt. Mpango

Ameongeza kuwa, kati ya taaisis hizo, taaisisi za Umma ni 495 na taasisi binafsi ni 267.

Makamu wa Rais amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kuendeleza na kusukuma matumizi ya nishati safi ya kupikia Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Sambamba na hilo Dkt. Mpango amezipongeza taasisi zote zilizotekeleza katazo hilo la kutotumia nishati isiyo safi na kutoa rai kwa taasisi ambazo hazijatekeleza agizo hilo ziendelee kuwekeza katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katika hafla hiyo ya Siku ya Mazingira dunian, Dkt. Mpango ametoa Tuzo kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati ikiwa upande wa REA tuzo imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bw. Renatus Msangira tuzo ya kutambua mchango wa REA katika kutunza mazingira kupitia utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia.

Miradi hiyo ambayo ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ni pamoja na usambazaji wa mitungi ya gesi pamoja na majiko banifu kwa bei ya ruzuku kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia vijijini.

Aidha, TANESCO tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange,ikiwa ni kutambua mchango wa TANESCO katika kuhifadhi mazingira kupitia utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ambao umeendelea kuzingatia misingi ya utunzaji wa mazingira sambamba na kuchangia kupunguza gesi joto.

Huku, CPA Mussa M. Makame - Mkurugenzi Mtendaji TPDC, amepokea TUZO ya kutambua mchango wa TPDC katika kuhifadhina kutunza mazingiza kupitia matumizi ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG).