TIMU YA PETE YA WANAWAKE YA WIZARA YA NISHATI YAENDELEA KUNG’ARA SHIMIWI 2026
Timu ya Pete ya Wanawake ya Wizara ya Nishati imeendelea kuonyesha ushindani katika Michuano ya SHIMIWI 2026, baada ya kutoka sare ya mabao 25–25 dhidi ya Timu ya Mashitaka katika mchezo wa leo.
Katika mchezo wa jana, timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 28–20 dhidi ya RAS Mara, na hivyo kuendelea kujijengea nafasi nzuri katika michuano hiyo.
Matokeo hayo yanaonesha dhamira, mshikamano na ushindani wa Timu ya Pete ya Wanawake ya Wizara ya Nishati katika michuano ya SHIMIWI mwaka huu.