Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​WAKILI BYABATO ASHIRIKI WIKI...

​WAKILI BYABATO ASHIRIKI WIKI YA MAFUTA AFRIKA NA KONGAMANO LA NISHATI RAFIKI NCHINI AFRIKA YA KUSINI

WAKILI BYABATO ASHIRIKI WIKI YA MAFUTA AFRIKA NA KONGAMANO LA NISHATI RAFIKI NCHINI AFRIKA YA KUSINI*

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameshiriki katika Wiki ya Mafuta Afrika (Africa Oil Week) na Kongamano la Nishati Rafiki (Green Energy Summit), jijini Cape Town, nchini Afrika Kusini.

Mikutano hiyo ilianza tarehe 03 Oktoba 2022 na itamalizika tarehe 07 Oktoba 2022.

Katika mikutano hiyo masuala mbalimbali yanajadiliwa ikiwemo Mafuta na Gesi Afrika pamoja na Nishati Salama Afrika. Mikutano hiyo imeandaliwa na Kamisheni ya Nishati Afrika (AFREC), Wiki ya Mafuta Afrika na Kongamano la Nishati Rafiki ambapo viongozi wa AFREC, Mawaziri, Mashirika ya Mafuta ya Kiserikali, Taasisi Mbalimbali Afrika na Kimataifa na Sekta Binafisi wamehudhuria.

Naibu Waziri Byabato katika mikutano hiyo ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Balozi Ombeni Sefue, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng'i Issa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mha. Charles Sangweni na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na TPDC.