Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

WATAALAM WA UFUATILIAJI NA TAT...

WATAALAM WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WIZARA YA NISHATI WASHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA UFUATILIAJI NA TATHMINI

Wataalam kutoka Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Nishati wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo hicho Bi. Anitha Ishengoma, wameshiriki Kongamano la Nne la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika jijini Mwanza.

Kongamano hilo lililoanza leo Septemba 10, 2025, limewakutanisha wataalam wa ufuatiliaji na tathmini kutoka Serikalini, Sekta binafsi na Washirika wa Maendeleo.

Lengo kuu la Kongamano hilo ni kujengeana uwezo na kujadili mbinu bora zitakazosaidia kuimarisha utekelezaji wa afua za maendeleo na kuongeza uwajibikaji katika sekta za umma na binafsi.

Kongamano hilo pia linatarajiwa kuchochea mabadiliko chanya katika namna ambavyo taasisi mbalimbali nchini zinavyotekeleza na kufuatilia miradi ya maendeleo huku msisitizo ukiwa katika kujenga utamaduni wa ufuatiliaji na tathmini katika shughuli za Serikali.

Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni "Kuimarisha Uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Jamii ili Kuwezesha Utendaji Bora na Maendeleo Endelevu.”

Kongamano litazinduliwa tarehe 11 Septemba, 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.