Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​Watumishi watakiwa kufahamu m...

​Watumishi watakiwa kufahamu maendeleo ya michango yao kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Watumishi watakiwa kufahamu maendeleo ya michango yao kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Watumishi wa Wizara ya Nishati wametakiwa kujenga utamaduni wa kufahamu maendeleo ya michango wanayochanga katika Mifuko wa Hifadhi ya Jamii ili kuondoa changamoto za upatikanaji mafao wakati wa kustaafu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba wakati wa kikao chake na Watumishi wa Wizara ya Nishati kilichofanyika jijini Dodoma, Februari 8, 2023.

“Watumishi jengeni utamaduni wa kufahamu maendeleo ya michango yenu katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kufahamu kama michango yenu inapelekwa kwa wakati katika mifuko hiyo pamoja na kiasi mlichochangia.” Amesema Mramba

Vilevile, Mhandisi Mramba ameitaka Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kuendelea kutengeneza utaratibu mzuri wa kuboresha utunzaji wa taarifa za Watumishi ili kuondoa changamoto pindi utumishi wao unapofikia kikomo na taarifa za kiutumishi zinapotakiwa katika mifuko ya kijamii.

Mhandisi Mramba pia aliwaasa Watumishi kufanya kazi kwa kujituma ili kuwa na tija katika sehemu ya kazi.

Katika kikao hicho masuala mbalimbali kuhusu Watumishi wa Wizara ya Nishati yalijadiliwa.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Menejimenti ya Wizara ya Nishati ikiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ziana Mlawa.