The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WAZAZI WAHAMASISHWA KUUNGA MKO...

WAZAZI WAHAMASISHWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT. SAMIA KWA KUCHANGIA SHULE ILI UENDELEZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Mkurugenzi Wa Nishati Safi Ya Kupikia Kutoka Wizara ya Nishati, Bw. Nolasco Mlay amewahimiza Wazazi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake watumie nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono jitihada na dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha ifikapo Mwaka 2034 asilimia 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati hiyo.

Amesema hayo aliposhiriki ziara ya kukagua Utekelezaji wa Maagizo Kutoka Ofisi ya Makamu ya Rais ya kuhakikisha Kuwa Kila Taasisi inahohudumia Watu zaidi ya 100 wanatumia Nishati safi katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha leo tarehe 29 Januari, 2026.

Amesema umefika wakati sasa wa Wazazi kutumia nishati safi ya kupikia badala ya kutafuta gunia la mkaa ama kuni.

"Mazingira ndio ajenda ya dunia, na Rais Wetu ndio Kinara wa Matumizi ya Nishati Safi maana yake tuunge mkono juhudi zake, tukae tujadili tuone namna ambavyo tutaweza kuwatoa wananchi kwenye dhana ya kutumia nishati isiyo Salama ya kuni na mkaa na kuwaleta kwenye nishati iliyo safi ya kupikia,” amesisitiza.

Pia, amewashukuru Viongozi wa Halmashauri Ya Wilaya ya Monduli kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha Serikali kwa kutekeleza Agizo la Kutumia Nishati Safi Ya Kupikia.

Amesema sio rahisi Serikali kujua kila sehemu yenye changamoto hivyo Viongozi wa Halmashauri wanafanya jitihada bila ya kulipwa na wanafichua maeneo yenye changamoto.

Amesisitiza Serikali inatambua na kuwashukuru wanapowasilisha changamoto hizo na kuzifanyia kazi.