The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

Waziri Ndejembi Awasili Mtwara...

Waziri Ndejembi Awasili Mtwara Kukagua Miradi ya Umeme

Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amewasili mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme. Akiwasili Machi 07, 2026 amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Donald Mséngi

Mara baada ya kuwasili, Waziri Ndejembi amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Leonard Akwilapo ambaye pia yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi.

Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya umeme ikiwemo Kituo cha Kupoza Umeme cha Mahumbika, ujenzi wa laini ya umeme ya Songea–Tunduru–Masasi, pamoja na Kituo cha Kupoza Umeme cha Tunduru. Pia atapata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa laini ya umeme ya Songea –Tunduru – Masasi inayolenga kuboresha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.