The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

WAZIRI WA NISHATI AMEKUTANA NA...

WAZIRI WA NISHATI AMEKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA EACOP

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ( EACOP), Bw. Guillaume Dulout katika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

Kikao hicho kimefanyika Januari 19, 2026 ambapo Kiongozi huyo wa EACOP alimtembelea Mhe Waziri Ndejembi kwa lengo la kujitambulisha kwake lakini pia kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano baina ya Wizara na EACOP.