Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

WIZARA YA NISHATI YAPOKEA MAGA...

WIZARA YA NISHATI YAPOKEA MAGARI KUTOKA MRADI WA UMEME WA NYAKANAZI

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Bi Ziana Mlawa ameongoza Watendaji mbalimbalikupokea magari sita kutoka Mradi wa Usafirishaji wa Umeme Nyakanazi katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba jijini Dodoma Leo Januari 09, 2025.

Katikamagari hayo sita yaliyopokelewa, moja litaenda Wizara ya Fedha,mawili yataenda Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

na magari matatu yatabaki Wizara ya Nishati.